1. UTANGULIZI
A-hijra Islamic Primary School inamilikiwa na Taasisi ya ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTER ambayo ina amini kuwa elimu ni jambo lenye umuhimu wa kwanza kwa Mwanadamu. Tunajifunza katika Qur’an kuwa Nabii Adamu (Alayhi ssalam) alielimishwa kwanza mazingira atakayoishi hapa duniani (Qur’an 2:31). Vilevile Mtume Muhammad (Swallallahu alayhi wasallam.) kabla ya kazi yake kubwa ya kuhuisha Uislam, alipewa amri ya kusoma kwanza (Qur’an 96:1-5).
2. LENGO LA SHULE NA MASOMO
Al-hijra Islamic Primary School ina malengo ya ujumla yafuatayo: -
-
Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa Kiislam (kike na kiume) ili wawe Waislam na raia wema watakaotoa mchango mkubwa kwa Taifa na Ummah wa Kiislam kwa ujumla.
-
Kuwaandaa vijana wa Kiislam kuwa viongozi waadilifu wa kutegemewa na Taifa na jamii ya Kiislam kwa ujumla.
SEKULA
- Civic and moral education
- Kiswahili
- English language
- Mathematics
- Social studies and vocational skills
- Science and technology
DINI
- Tah-fidhil Qur’an
- Tarbiya
- Fiqhi
- Sira
- Tawhiid
- Hadithi
- Arabic language
- Adh-kar
3. MAENDELEO YA DARASANI
- Kila Mwanafunzi analazimika kufanya bidii katika masomo yote. Mwanafunzi mvivu hatavumiliwa
- Mwanafunzi wa darasa la tatu hadi darasa la sita hata ruhusiwa kuingia darasa linalofuata bila kupata wastani wa 31(B) au zaidi kutokana na mitihani yote aliyoifanya mwisho wa mwaka.
- Kujibidiisha katika kazi ni katika nidhamu ya Kiislam hivyo, kila Mwanafunzi atawajibika kushiriki kikamilifu katika kutenda kazi za usafi wa mazingira na kazi nyingine kama atakavyo elekezwa na Walimu au Viongozi wa Wanafunzi. Kutegea kazi ya darasani au nje ya darasa ni kukiuka maadili anayotarajiwa awe nayo Mwanafunzi wa Shule hii na Shule haitamvumilia.
4. SARE YA SHULE
Wanafunzi watakaodahiliwa shuleni hapa hawataruhusiwa kuja na nguo zaidi ya zitakazo ainishwa katika jedwali lifuatalo;
4. VIFAA VYA MASOMO NA BWENINI VINATOLEWA SHULENI
Kila mwanafunzi analazimika kuwa na vifaa vya masomo ambavyo vitatolewa na shule gharama (199,000/=) imeainishwa hapo chini;
- Godoro 45,000/=
- Shuka 2 = 16,000/=
- Trunk 25,000/=
- Daftari 15 (3 Quires 10 @ 3,000 na 4 Quire 5 @ 3,500)
- Chandarua 12,000/=
- Rimu A4 16,000/= na Rimu ya mistari 9,000/=
- Mkebe 2,500
- Jembe na mpini 8,000
- Ndoo, beseni,sahani, kikombe na bakuli 10,000
- Graph paper 2 @ 2,500
- Seti ya penseli za rangi 3,000
5. VIFAA VYA HOSTELI
- Taulo, malapa na mswaki.
- Chupa ya kuhifadhia maji ya moto
- Sabuni ya kufulia na kuogea.
- Sweta la kufuma rangi blue (kuvaa wakati wa baridi)
- Mini Whiteboard 1, Past it Note dozen 1
- Msahafu
- Mkoba wa Madaftari (Begi Jeusi)
- Kalamu za kutosha
6. ADA NA MICHANGO YA SHULE
Mwanafunzi anatakiwa kulipa ada ya shule ya mwaka wa masomo 2023 kwa utaratibu ufuatao,
2. Awamu ya pili: Januray (Tsh. 650,000/=)
3. Awamu ya tatu: Januray (Tsh. 400,000/=)
- Alipe ada yote kwa mwaka Tsh 1,850,000/=
- Alipe kwa awamu tatu kama inavyoainishwa katika jedwali hapo chini. Malipo Yanafanywa Wiki ya Kwanza ya Mwezi Tajwa
2. Awamu ya pili: Januray (Tsh. 650,000/=)
3. Awamu ya tatu: Januray (Tsh. 400,000/=)
- Mwanafunzi ambaye hana bima ya afya aje na shilingi elfu sitini (60,000/=) kwa ajili ya kulipia bima hiyo.
- Wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023 wanalazimika kulipa 250,000/= kwa ajili ya iPad (Kishikwambi) kwa kuwa ufundishaji na ujifunzaji utatumia teknolojia.
- Malipo ya ada yafanyike kupitia AMANA BANK Akaunti Namba 008121053180001 au DIAMOND TRUST BANK (DTB) Akaunti Namba 0035678001, Jina la Akaunti PONGWE ISLAMIC GIRLS SECONDARY SCHOOL.
7. UANDIKISHWAJI
Siku ya kuripoti shuleni mwanafunzi awe na vifaa vifuatavyo:
- Fomu za maelezo ya mzazi / mlezi kuhusu utambulisho wa mwanafunzi na wazazi / walezi (Kiambatanisho A)
- Maelezo yaliyothibitishwa na Daktari (Medical Examination Report) kama mwanafunzi ana matatizo ya kiafya au la (Kiambatanisho B).
- Stakabadhi ya Malipo ya Benki (Pay in Slip)
- Rimu mbili (2), (A4) moja na Karatasi zenye mistari (Ruled Paper) moja.
- Picha tatu (3) za passport size au TShs 2000/=.
- Uthibitisho wa Kumaliza Darasa la Saba (VII) (Namba ya PLSE)
- Fagio la njiti, jembe na mpini kwa ajili ya usafi wa mazingira.
- Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.
8. MAENDELEO YA DARASANI
Ili kufaulu kuingia Kidato II mwanafunzi anatakiwa afikishe wastani wa alama zisizopungua 55% na Credit saba (7) au zaidi kwa mwanafunzi atakaeingia Kidato IV. Somo la Maarifa ya Uislamu na Lugha ya Kiarabu yanachukua uzito wa pekee hivyo kila mwanafunzi analazimika kufanya bidii na kuhakikisha anafaulu angalau kwa kiwango cha daraja ‘B’.
9. KUTEUA MASOMO
-
Mwanafunzi atakayefaulu kuingia Kidato cha Tatu atachagua masomo katika mchepuo wa Sayansi na Sanaa (Arts) tu.
-
Uchaguzi wa masomo utazingatia uwezo wa mwanafunzi, utashi wake, ushauri wa Wazazi/Walezi na waalimu wa masomo husika atakuwa na nafasi kubwa zaidi katika maamuzi hayo.
10. KUTEMBELEA WANAFUNZI
Shule inatoa fursa kwa wazazi /walezi kutembelea wanafunzi kila Jumapili ya mwisho wa mwezi isipokuwa kipindi cha mitihani. Pamoja na ruhusa hiyo mzazi/ mlezi haruhusiwi kumletea mwanafunzi chakula cha aina yoyote.
11. KANUNI NA MWENENDO BORA WA SHULE
- Wanafunzi wote wanapaswa kufahamu kuwa chochote kilicho nje ya maadili mema hakina nafasi hapa shuleni.
- Kila mwanafunzi hana budi kujipamba na vipengele vya tabia njema.
- Kila mwanafunzi atawajibika kuzingatia na kufuata kikamilifu ratiba na kalenda ya shule.
- Mwanafunzi atakuwa kajifukuzisha shule mwenyewe iwapo hatafika shule kwa siku ishirini na moja (21) bila taarifa zozote shuleni. Taarifa iwe kabla na wala si baada ya tukio la utoro.
- Wakati wa masomo wanafunzi wote watabaki shuleni, hawataruhusiwa kutoka ndani ya shule isipokuwa kwa kibali maalum.
- Mwanafunzi atakaekuwa na Wastani wa mahudhurio chini ya asilimia themanini na moja (81%) hatoruhusiwa kufanya mtihani, hivyo hatoruhusiwa pia kuendelea na Kidato kinachofuata, baadala yake atarudia mwaka au kufukuzwa shule.
- Wakati wote wa kuwa shule, vazi rasmi ni sare ya shule, kinyume chake ni kosa. Mwanafunzi atavaa na kuzingatia maadili hata awapo nje ya shule.
- Mwanafunzi ataripoti tatizo kwanza kwa Head Girl kisha ndipo amwone Mwalimu wa zamu, darasa au nidhamu.
- Kelele au zogo hairuhusiwi katika eneo la shule, mazungumzo yote hayanabudi kufuata nidhamu na maadili.
- Hairuhusiwi wanafunzi kuja shuleni na chakula cha aina yoyote ama kuletewa zawadi ya chakula na mzazi/mlezi wakati atakapotembelewa.
- Ni marufuku kwa mwanafunzi kujipamba kwa rangi za kucha, nywele, midomo, kupaka wanja, kunyoa nyusi, kuvaa hereni, bangili, mkufu au pete.
- Hairuhusiwi kufanya sherehe za Birtdhday na au Valentine Day kwa namna yoyote shuleni.
- Hairihusiwi kulala zaidi ya mwanafunzi mmoja katika kitanda kimoja.
- Vifaa vya electronics kama vile simu au line, mp3, ipod, camera, radio, radio cassette n.k haviruhusiwi mwanafunzi kuwa navyo katika mazingira ya shule.
- Mbali na kuvunja kanuni hizi halali za shule mwanafunzi atajifukuzisha shule mwenyewe iwapo atajihusisha na ulevi, uesherati na uzinifu.
❖ Mamlaka ya shule ndio yenye maamuzi ya mwisho katika kutekeleza kanuni hizi.
12. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE
Pamoja na maelezo yote hayo. Mwanafunzi atakayechupa kwa makusudi maadili na kanuni za shule kwa kutenda makosa makubwa kama yalivyoainishwa hapo chini atafukuzwa shule:
- Kunywa pombe
- Kwenda nyumba za starehe kama vile kwenye kumbi za madansi, disko n.k
- Uzinzi,ushoga au kukaribia zinaa kwa namna yeyote.
- Kuvuta bangi, madawa ya kulevya, n.k
- Kutosimamisha swala.
- Kumiliki vitu vya electronics kama simu au line, mp3, ipod, radio, kamera n.k
- Kutoroka shuleni
- Kugoma adhabu stahiki kwa makusudi.
- Kupata mimba au kutoa mimba ndani na nje ya shule
- Kuanzisha, kuchochea, kushiriki au kuongoza mgomo.
- Kuhatarisha amani ya shule kwa kupigana au kuchochea watu wapigane
- Wizi, uporaji na uharibifu wa mali ya shule na ya wanafunzi au wakazi wa kituo.
- Kukosa mitihani/jaribio bila ya sababu za msingi.
- Kutohudhuria masomo/darasani bila sababu maalumu za msingi.
13. HITIMISHO
Ni matumaini yetu kuwa Mzazi/ Mlezi na mwanafunzi mtarajiwa mmeyasoma maelezo haya kwa makini tayari kwa utekelezaji.
Baada ya kujiunga na shule utekelezaji wa kanuni na taratibu za shule kwa mwanafunzi na Mzazi/Mlezi ni wajibu.
Mzazi / Mlezi mlete mwanao PONGWE ISLAMIC GIRLS SECONDARY SCHOOL yenye mazingira mazuri ya kimalezi ili aweze kupata masomo na maadili mema kwa maslahi ya mtoto, wazazi, na jamii kwa ujumla.
TUNAKUTAKIA MAISHA MEMA NA KARIBU SANA
Baada ya kujiunga na shule utekelezaji wa kanuni na taratibu za shule kwa mwanafunzi na Mzazi/Mlezi ni wajibu.
Mzazi / Mlezi mlete mwanao PONGWE ISLAMIC GIRLS SECONDARY SCHOOL yenye mazingira mazuri ya kimalezi ili aweze kupata masomo na maadili mema kwa maslahi ya mtoto, wazazi, na jamii kwa ujumla.
TUNAKUTAKIA MAISHA MEMA NA KARIBU SANA